Jinsi mfumo unavyofanya kazi

Muhtasari kwa msomaji na mwandishi — Simulizi Hub ni huduma inayomilikiwa na Swaxnet (kama ilivyoelezwa katika Sera ya Faragha).

Simulizi Hub ni nini?

Ni jukwaa la mtandao unapoweza kusoma na kuandika simulizi za Kiswahili. Kila “simulizi” inaweza kugawanywa kwa sehemu (episodes). Mwandishi anaweza kuweka maandishi, sauti, faili ya PDF, au Excel kwa sehemu moja moja.

Kama msomaji

  1. Tembelea ukurasa wa nyumbani, tafuta, au waandishi kupata hadithi.
  2. Simulizi bure hufunguka kwa kila mtu. Simulizi za kulipia zinahitaji malipo au sehemu za “preview” zilizo wazi.
  3. Kitufe cha Hifadhi (favorites) kinakuwezesha kurudi simulizi unazopenda kwa urahisi.
  4. Unapo hifadhi simulizi, tunaweza kukutumia arifa kwa barua pepe sehemu mpya inapochapishwa (kama umejisajili na barua pepe iko sawa).
  5. Unaweza kuripoti maudhui yanayokukera kwenye ukurasa wa simulizi au sehemu — timu ita pitia repoti yako na kuifanyia kazi kwa wakati.

Kama mwandishi

  1. Unda simulizi, weka jalada na maelezo, kisha ongeza sehemu moja moja.
  2. Unaweza kuweka bei simulizi ikiwa unataka mapato kupitia malipo ya simu (kulingana na mipangilio ya jukwaa).
  3. Kwenye dashboard unaona muhtasari wa maoni, mapato ya hivi karibuni, na jumla ya mapato kwa mwezi (kutokana na miamala iliyothibitishwa).
  4. Alama ya uaminifu (bluu) inatolewa na msimamizi baada ya uhakiki — si kiotomatiki.

Simulizi Plus (bila matangazo)

Kwa watumiaji walio na Simulizi Plus (kwa muda maalum), matangazo ya nje yanaweza kuzimwa ili uzoefu usiwe mzito. Muda wa huduma huu huongezwa na msimamizi au mipango ya malipo ya baadaye. Ukiona ujumbe wa Plus kwenye profaili yako, bado una huduma hiyo hadi tarehe iliyoonyeshwa.

Usalama, faragha, na mali ya kifedha

Taarifa zako binafsi na jinsi tunavyozitumia zinaelezwa katika Sera ya Faragha. Masharti ya matumizi yapo katika Masharti ya Huduma. Malipo na mapato yanasimamiwa kwa njia zilizounganishwa kwenye mfumo — si kwa kukopa namba za kadi kwenye jukwaa hili.

Kwa nini kurasa zinaweza kuchelewa?

Matukio ya kawaida ni mtandao dhaifu, simu za bei nafuu, picha nyingi za jalada zinazopakiwa pamoja, na matangazo ya nje (kama yamewashwa na hayajaondolewa na Plus). Tunaweza kuhifadhi kwa muda fupi orodha za nyumbani ili kupunguza mzigo kwenye seva — mabadiliko ya simulizi yanaonyesha orodha mpya baada ya muda mfupi.

Programu ya simu (PWA na APK)

Unaweza kuongeza Simulizi Hub kwenye skrini ya simu kutoka kivinjari (ongeza kwenye skrini ya nyumbani). Ikiwa hakuna intaneti, utaona ujumbe wazi badala ya ukurasa tupu. Kiungo cha APK (Android) kinapatikana menyu ikiwa kimepangwa na msimamizi.

Utafutaji na kushiriki

Tovuti ina ramani ya kurasa (sitemap) inayosaidia injini za utafutaji. Kurasa za simulizi zina maelezo maalum kwa mitandao ya kijamii na utafutaji — ikiwa unashiriki kiungo, kielelezo kinaweza kuonyesha jalada la hadithi husika.

Kuhakikisha arifa zinafika kwa wakati

Ili barua nyingi zisizidi kuchelewesha jukwaa, arifa za sehemu mpya hupangwa kupitia foleni ya ujumbe kwenye seva. Msimamizi wa kiufundi anahakikisha huduma hiyo inaendelea kufanya kazi kila wakati kwenye mazingira ya uzalishaji.

Profaili

Alama ya uaminifu