Mapenzi Kwenye Mstari Mwembamba

Sehemu 2

EPISODE 2: Siri Inaanza Kufichuka

Mapenzi Kwenye Mstari Mwembamba • Aisha Mtamu

Sikiliza Audio:

Asubuhi ilifika, lakini kwa Mariamu haikuwa asubuhi ya kawaida.
Usiku mzima hakulala.
Ujumbe aliouona kwenye simu ya Benjamini uliendelea kumzunguka kichwani kama ndoto mbaya isiyoisha.
"Nakumiss… lini utaniona tena?"
Alijiuliza maswali mengi… Ni nani huyo “S”? Tangu lini? Na kwa nini Benjamini amekuwa tofauti hivi?
Alipokuwa jikoni akipika chai, Benjamini alitoka chumbani akiwa tayari kwenda kazini.
“Mariamu, chai iko?” aliuliza kawaida kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea.
Mariamu alimwangalia kwa macho ya uchungu lakini akajizuia.
“Ipo,” alijibu kwa kifupi.
Kulikuwa na ukimya mzito kati yao.
Benjamini alihisi kuna kitu, lakini hakujua ni nini hasa Mariamu amegundua.
Wakati huo huo…
Johnson alikuwa kazini lakini akili yake haikuwa sawa. Simu ya Mariamu ya jana usiku haikuwa ya kawaida.
Alimtext:
"Vipi Mariamu, kuna shida?"
Dakika chache baadaye jibu likaja:
"Nahitaji kuonana na wewe. Ni muhimu."
Moyo wa Johnson ulianza kwenda mbio.
Upande wa Neema…
Alikuwa amekaa na rafiki yake wa karibu, Asha, wakinywa kahawa.
“Neema, siku hizi unaonekana kama una mawazo mengi,” Asha alisema.
Neema alitabasamu kwa kulazimisha, “Hakuna kitu kikubwa…”
Lakini ukweli ni kwamba Neema alikuwa anahisi kuna kitu kinabadilika kwa mume wake Johnson.
Simu nyingi, kutoka nje mara kwa mara… na sasa alikuwa anaficha mambo.
Mchana huo…
Mariamu alikutana na Johnson sehemu ya faragha, mbali na watu.
Johnson alipofika, alimkuta Mariamu tayari amekaa, uso wake ukiwa umejaa huzuni.
“Mariamu, kuna nini?” Johnson aliuliza kwa wasiwasi.
Mariamu hakupoteza muda.
Alimkabidhi simu yake, akamuonyesha ujumbe ule ule.
Johnson aliposoma… uso wake ulibadilika ghafla.
“Mariamu… hii umeipata wapi?” aliuliza kwa sauti ya chini.
“Ni kwenye simu ya Benjamini,” Mariamu alisema kwa uchungu.
Kulikuwa na ukimya mfupi.
Kisha Mariamu akaongeza:
“Naomba uniambie ukweli… huyu ‘S’ ni nani?”
Johnson alikaa kimya kwa sekunde kadhaa… akimeza mate.
Kitu ambacho Mariamu hakukitegemea kilitoka kinywani mwake:
“...Ninamfahamu.”
Mariamu alishtuka.
“Nini?!”
Wakati huo huo…
Peter Joram alikuwa live kwenye blog yake, akizungumzia:
"Wanaume wawili, rafiki mmoja, na mwanamke mmoja katikati… hii story sio ya kawaida."
Post yake ilianza kusambaa kwa kasi.
Kastul, mwandishi wa habari, alitazama hiyo post na kusema kwa sauti:
“Hii sio story ya kubuni… kuna mtu anaumia kweli hapa.”
Kurudi kwa Mariamu na Johnson…
“Mariamu… jambo hili ni kubwa kuliko unavyofikiria,” Johnson alisema kwa sauti nzito.
“Basi niambie ukweli!” Mariamu alipaza sauti.
Johnson akavuta pumzi ndefu…
“Yule ‘S’… anaitwa Sophia.”
Mariamu alihisi dunia inazunguka.
Lakini hakujua bado…
Sophia hakuwa mtu wa mbali.
Alikuwa mtu wa karibu sana…
👉 Episode 3 itakuwa hatari zaidi: Tutafichua Sophia ni nani hasa, na connection yake na Benjamini, Johnson na Neema 😳

Maoni

Hakuna maoni bado

Profaili

Alama ya uaminifu