Juma. EPISODE 5: Hisa ya Kwanza
SEASON 2: Kutoka Biashara Hadi DSE • Aisha Mtamu
Hatua ya kwanza huwa na hofu… lakini pia ndiyo inayofungua milango.“Nunua kwa laki mbili,” Juma alisema. Hiyo ilikuwa pesa ambayo aliiheshimu sana. Sio ndogo kwake. Dakika chache baadaye… Muamala ukafanyika. Juma akaangalia simu yake… Alikuwa rasmi amewekeza. Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa. Hakujua kama afurahi… au aogope. Khalid akamgonga begani: “Hongera bro… sasa wewe ni investor.” Lakini safari haikuishia hapo… Siku chache baadaye… Juma alifungua tena simu yake kuangalia hisa zake. Alitarajia kuona faida… Lakini alichokiona kilimfanya ashangae. Bei ilikuwa imeshuka. Moyo wake ulishtuka. “Bro… pesa yangu imepungua!” alisema kwa hofu.
Soko la hisa halitembei moja kwa moja juu… hupanda na kushuka.Juma alianza kupata mawazo mengi: “Niuze sasa?” “Nisubiri?” “Je, nimekosea?” Alimpigia Khalid haraka. “Bro, bei imeshuka… nifanye nini?” Khalid akamjibu kwa utulivu: “Swali sio bei imeshuka… swali ni umewekeza kwenye kampuni nzuri?” Juma akakumbuka alichojifunza. Ndiyo… alikuwa amechagua kwa uelewa.
NOTE: Kushuka kwa bei kwa muda mfupi sio hasara halisi — ni sehemu ya kawaida ya soko.
Khalid akaendelea: “Ukianza kuuza kila bei ikishuka… hutawahi kushinda kwenye uwekezaji.” Juma alikaa kimya. Alikuwa anajifunza kitu muhimu sana… Uvumilivu. Aliamua kufanya kitu ambacho wengi hushindwa kufanya… Hakuuza.Uwekezaji wa kweli haupimwi kwa siku… unapimwa kwa muda.Siku zikapita… Bei ikaendelea kupanda na kushuka… Lakini safari hii Juma hakuwa na panic kama mwanzo. Alianza kuelewa mchezo. Lakini bado kulikuwa na hatua nyingine muhimu sana… Kupata faida ya kwanza (dividend). 👉 Episode 6 itakuwa ya 🔥