EPISODE 10: Akili ya Mfanyabiashara (Finale)
Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu
Uzoefu ndio mtaji mkubwa kuliko pesa.Jioni hiyo, Khalid alimtembelea. “Bro, sasa unaonekana mfanyabiashara kweli,” alisema kwa furaha. Juma akacheka kidogo. “Safari imenifunza sana…” Khalid akamuuliza swali la mwisho: “Sasa unajua siri ya biashara?” Juma alikaa kimya kidogo… Kisha akasema:
Biashara sio bahati… ni nidhamu, maamuzi sahihi na uvumilivu.Khalid akatabasamu. “Umefika.” Juma hakuishia hapo… Alianza kufikiria mbali zaidi: Kufungua duka rasmi Kupanua biashara online Kujenga brand kubwa zaidi Lakini safari hii… Hakukimbilia. Alipanga.
NOTE: Mafanikio ya biashara hayatokani na haraka — yanatokana na consistency, nidhamu na maamuzi sahihi ya kila siku.
Siku moja… Kijana mmoja alimfuata Juma. “Bro, nataka nianze biashara… nifanyeje?” aliuliza. Juma alitabasamu. Aliona yeye wa zamani ndani yake. Akamuambia kwa utulivu:Anza na kidogo, jifunze kila siku, na usikate tamaa… biashara ni vita, lakini unaweza kushinda.Kijana aliondoka akiwa na matumaini. Juma akabaki akitazama mbele… Safari ilikuwa bado inaendelea. Lakini sasa… Alikuwa tayari. Hapa ni mwisho wa Season 1 Tukutane SEASON 2: Kutoka Biashara Hadi DSE