EPISODE 2: Hofu na Ukweli
SEASON 2: Kutoka Biashara Hadi DSE • Aisha Mtamu
Kwenye uwekezaji, sauti nyingi zinaweza kukupoteza… lakini ukweli ni mmoja.Jioni hiyo… Alikutana na Khalid tena. “Bro, nimeona watu wengine wanasema DSE ni scam…” Juma alisema kwa wasiwasi. Khalid akacheka kidogo. “Kila kitu ambacho hujaelewa, kitaonekana kama scam.” Juma akakaa kimya. “Kwa hiyo sio scam?” aliuliza. Khalid akamjibu kwa utulivu: “Hapana. Lakini sio rahisi kama watu wanavyofikiria.”
Uwekezaji sio mchezo wa bahati… ni mchezo wa maarifa na uvumilivu.Khalid akaanza kuvunja ukweli mmoja baada ya mwingine: Soko linaweza kupanda na kushuka Unaweza kupata faida… au hasara Hakuna pesa ya haraka (get rich quick) Juma alimsikiliza kwa makini. Kwa mara ya kwanza… Alianza kuelewa kuwa hii sio shortcut.
NOTE: Uwekezaji wa kweli haukupi pesa haraka — unakujengea utajiri polepole kwa muda mrefu.
Lakini bado kulikuwa na swali kubwa moyoni mwa Juma… “Na kama nikipoteza pesa je?” Khalid akamwangalia moja kwa moja… Kisha akasema:Hasara sio kushindwa… ni sehemu ya kujifunza kwenye uwekezaji.Maneno hayo yalimpa Juma utulivu kidogo. Sio kwamba hofu ilipotea… Lakini ilianza kupungua. “Kwa hiyo nianzie wapi?” Juma aliuliza. Khalid akatabasamu. “Hatua ya kwanza ni kufungua akaunti ya uwekezaji.” Juma akashangaa. “Akaunti tena?” Khalid akasema: “Ndiyo… bila akaunti huwezi hata kuanza.”
Kila safari ya uwekezaji huanza na hatua moja ndogo — kujiandaa.Juma alikubali. Safari sasa ilikuwa rasmi imeanza. 👉 Episode 3 itakuwa ya vitendo kabisa 🔥