SEASON 2: Kutoka Biashara Hadi DSE

Sehemu 3

EPISODE 3: Kufungua Akaunti (CDS)

SEASON 2: Kutoka Biashara Hadi DSE • Aisha Mtamu

Asubuhi hiyo, Juma alikuwa na hamasa tofauti. Safari hii hakutaka kusikia tu… Alitaka kuanza kweli. Alikutana na Khalid mapema. “Bro, leo nataka kufungua hiyo akaunti,” Juma alisema kwa kujiamini. Khalid akatabasamu. “Hapo sasa unaanza kuwa serious.” Wakaelekea ofisi ya broker anayehusika na Dar es Salaam Stock Exchange. Juma alikuwa kimya njiani… Alikuwa anahisi kama anaingia dunia mpya kabisa. Walipofika… Walipokelewa na afisa mmoja. Akawaeleza kwa utulivu: “Ili uanze kununua hisa, lazima uwe na CDS Account (Central Depository System).” Juma alisikiliza kwa makini. Huwezi kuwekeza bila mfumo — CDS ndio mlango wa kuingia kwenye soko la hisa. Afisa akaanza kumueleza Juma vitu vinavyohitajika: Kitambulisho (NIDA / Passport) Namba ya simu Email address Maelezo ya benki Juma akashangaa. “Kwahiyo sio ngumu?” aliuliza. Afisa akatabasamu: “Ni rahisi kama kufungua akaunti ya benki.” Juma akaanza kujaza fomu. Alikuwa makini sana… Kila detail alihakikisha iko sahihi. Kwa sababu alijua… Hii sio mchezo. Dakika chache baadaye… Akaambiwa: “Hongera, akaunti yako ya CDS imefunguliwa.” Juma alihisi kitu tofauti ndani yake. Ilikuwa kama hatua kubwa ya maisha.

NOTE: Kufungua akaunti ya uwekezaji ni hatua ya kwanza muhimu — lakini sio mwisho. Maarifa ya jinsi ya kutumia akaunti hiyo ndio yatakayoamua mafanikio yako.

Walipotoka nje… Juma alimgeukia Khalid. “Bro… sasa nimeanza rasmi?” Khalid akacheka kidogo. “Umeingia uwanjani… lakini bado hujaanza kucheza.” Juma akakunja uso. “Inamaanisha?” Khalid akamwambia: Kufungua akaunti sio uwekezaji… kuchagua kampuni sahihi ndio mchezo halisi. Juma alielewa. Hatua inayofuata ilikuwa kubwa zaidi. Usiku huo… Alifungua simu yake… Akaanza kuangalia list ya kampuni zilizopo kwenye soko la hisa. Majina mengi… Takwimu nyingi… Hakuelewa vizuri bado. Alijiuliza: “Nianzie wapi?” Ndani yake alijua… Uamuzi atakaochukua hapa unaweza: Kumwingizia faida Au kumpotezea pesa Sio kila kampuni ni uwekezaji mzuri… kuchagua vibaya ni sawa na kupoteza pesa. 👉 Episode 4 itakuwa muhimu sana 🔥 Tutajifunza jinsi ya kuchagua kampuni (stocks) Difference kati ya kampuni nzuri na mbaya Na makosa makubwa ya beginners

Maoni

Hakuna maoni bado

Profaili

Alama ya uaminifu