EPISODE 3: Biashara Mtandaoni (Online)
Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu
Ukibaki ulipo, hutobadilisha maisha yako.Siku iliyofuata, Khalid alimsaidia kufungua akaunti ya WhatsApp Business na Instagram. “Hatua ya kwanza ni picha,” Khalid alisema. Juma akashangaa, “Picha tu?” Khalid akamjibu:
Wateja wa online hununua kwa macho kwanza kabla ya pesa.Juma alianza kupiga picha za nguo zake. Lakini kulikuwa na tatizo… Picha zilikuwa hazivutii: Zilikuwa na mwanga mdogo Background ilikuwa chafu Nguo hazikuonekana vizuri Matokeo yake? Hakuna aliyekuwa anauliza bei. Baada ya siku mbili za frustration… Khalid alirudi tena. “Bro, hii ndio inakuangusha,” alisema. Akamfundisha: Kupiga picha kwenye mwanga wa jua Kutumia background safi Kupanga nguo vizuri Kisha akamwambia:
Biashara online sio kuuza bidhaa tu… ni kuuza muonekano.Juma alichukua hatua. Siku hiyo hiyo alipiga picha mpya — safi, zenye mwanga, na zilizopangwa vizuri. Akaziweka status na Instagram. Dakika 30 baadaye… Mtu akamtext: “Hi, hiyo shati ni bei gani?” Juma alishangaa. Alijibu haraka. “Elf 12.” Mteja akasema: “Nipo Mbagala, unafikisha?” Juma alikaa kimya. Hakuwahi kufikiria delivery. Hapo ndipo changamoto mpya ilipoanza…
NOTE: Wafanyabiashara wengi huanza kuuza bila kufikiria logistics (usafirishaji). Hii inaweza kuharibu biashara yako mapema.
Juma alimtafuta Khalid tena. “Bro, mtu anataka delivery… nifanyeje?” Khalid akasema: “Usijali. Tumia bodaboda au courier.” “Na gharama je?” Juma aliuliza. Khalid akamwangalia moja kwa moja:Usipojua jinsi ya kupanga gharama zako, utauza sana lakini hutapata faida.Juma akakaa chini akaanza kuhesabu: Bei ya kununua nguo Faida yake Gharama ya delivery Hatimaye akampatia mteja jibu: “Delivery ni extra elf 3.” Mteja akasema: “Sawa, niletee.” Hii ilikuwa order yake ya kwanza online. Alijisikia kama amefungua mlango mpya wa maisha. Lakini hakujua… Online kuna changamoto nyingine kubwa zaidi: Wateja wanao-cancel order Wadanganyifu Na ushindani mkubwa zaidi
Biashara ikikua, changamoto pia hukua.
👉 Episode 4 itakuwa kali zaidi 🔥 Utajifunza kuhusu wateja wanaosumbua (fake customers) Na jinsi ya kuepuka hasara kwenye delivery