Biashara Ni Vita

Sehemu 4

EPISODE 4: Wateja wa Mtandaoni (Fake & Real)

Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu

Baada ya Juma kufanikiwa kufanya delivery yake ya kwanza, alijisikia kama amepiga hatua kubwa sana. Alianza kujiamini zaidi. Alipost bidhaa nyingi zaidi WhatsApp na Instagram. Ndani ya siku mbili… alipata messages nyingi sana. “Hi, hiyo shati ni bei gani?” “Una size L?” “Nitachukua kesho” Juma alifurahi. Alidhani biashara yake imeanza kushika moto. Lakini hakujua… Sio kila mteja anayekuuliza bei ana nia ya kununua. Siku iliyofuata… Mteja mmoja alimtext: “Bro, nataka mashati mawili, niletee Sinza.” Juma alifurahi sana. Hii ilikuwa order kubwa kwake. Aliandaa mzigo haraka… akachukua bodaboda. Alilipa delivery elf 4. Walipofika Sinza… Simu ya mteja haikupokelewa. Walipiga tena… Haipatikani. Juma alihisi tumbo linamuwaka. “Subiri kidogo labda atapiga,” alimwambia bodaboda. Dakika 20 zikapita… Hakuna jibu. Hatimaye… Alikubali ukweli mchungu. Alikuwa amechezewa. Alirudi nyumbani akiwa kimya sana. Hasara ilimuuma: Gharama ya delivery Muda wake Na matumaini yake Alimpigia Khalid. “Bro… nimepigwa,” alisema kwa sauti ya kukata tamaa. Khalid hakushangaa. Badala yake akasema: Karibu kwenye biashara ya online… hapa kuna wateja na kuna wachezaji. Juma alikasirika. “Sasa nifanyeje? Nitaendelea kupoteza pesa hivi?” Khalid akamwambia: “Lazima ubadilishe mfumo wako.” Khalid alimfundisha vitu muhimu: Usikubali delivery bila uthibitisho Chukua advance kidogo Hakiki namba ya mteja kabla ya kusafirisha

NOTE: Kwenye biashara ya online, usalama wa pesa zako ni muhimu kuliko kuuza haraka. Bora ukose mauzo kuliko kupata hasara.

Siku iliyofuata… Juma alijaribu mfumo mpya. Mteja alimtext: “Nahitaji shati, niletee.” Juma akajibu: “Sawa, lakini delivery ni baada ya kulipa advance kidogo.” Mteja akanyamaza. Dakika chache baadaye… Akatuma pesa. Juma alitabasamu. Huyu alikuwa mteja wa kweli. Ndani ya siku chache… Juma alianza kuelewa tofauti ya: Mteja wa kweli Na mtu wa kupoteza muda Biashara yake ilianza kuwa stable zaidi. Lakini bado… Kulikuwa na kitu kimoja kilikuwa kinamzuia kukua zaidi: Hakukuwa na brand. Watu walimjua kama muuzaji wa kawaida tu. Hakuna kitu kilimtofautisha. Kama huna utambulisho (brand), utashindana na kila mtu. 👉 Episode 5 itakuwa game changer 🔥 Tutajenga BRAND ya Juma Jina la biashara Na jinsi ya kuvutia wateja wengi zaidi

Maoni

Hakuna maoni bado

Profaili

Alama ya uaminifu