EPISODE 6: Pesa Zinaongea (Capital vs Profit)
Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu
Pesa zote unazoona sio faida… nyingine ni mtaji wako.Baada ya siku chache… Alitaka kwenda kununua mzigo mpya wa nguo. Alipohesabu pesa… Akashangaa. “Mbona haitoshi?” Moyo wake ulianza kwenda mbio. “Lakini nilikuwa na pesa nyingi…” Alimpigia Khalid haraka. “Bro, sijui nini kinaendelea… pesa imepotea!” Khalid alimuuliza swali moja tu: “Uliwahi kutenganisha faida na mtaji?” Juma alikaa kimya. Hakuwahi kufanya hivyo. Khalid akamwambia:
Ukichanganya mtaji na matumizi binafsi, biashara yako itaonekana inakua… lakini inakufa taratibu.Juma alihisi aibu. Lakini pia alijifunza. Khalid alimfundisha mfumo rahisi: 1. Mtaji (Capital) – pesa ya kununua mzigo 2. Faida (Profit) – pesa inayobaki baada ya gharama 3. Matumizi binafsi – pesa ya maisha
NOTE: Usitumie pesa ya biashara kama ATM. Jiwekee mfumo wa kujilipa (salary) ili biashara ikue.
Juma alichukua hatua. Alianza: Kuandika kila mauzo Kuandika kila matumizi Kutenganisha pesa Mwanzoni ilikuwa ngumu… Lakini polepole akaanza kuona tofauti. Baada ya wiki mbili… Aliweza kusema kwa uhakika: “Hii ndio faida yangu halisi.” Na kwa mara ya kwanza… Biashara yake ilianza kuwa chini ya control. Lakini kadri pesa zilivyoanza kuonekana… Kulikuwa na hatari nyingine kubwa zaidi ilianza kumkaribia: Mikopo na madeni.Sio kila pesa inayokuja kwako ni ya kuchukua… nyingine ni mtego.👉 Episode 7 itakuwa hatari sana 🔥 Tutazungumzia mikopo, madeni na washkaji wanaokukopesha Na jinsi watu wengi wanavyoanguka kwenye biashara