EPISODE 7: Mkopo – Msaada au Mtego?
Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu
Mkopo unaweza kukuinua haraka… au kukuangusha vibaya zaidi.Juma alimtafuta Khalid tena. “Bro, nimepata chance ya mkopo… nichukue?” aliuliza. Khalid hakujibu haraka. Alimwangalia Juma kwa makini, kisha akamuuliza: “Una uhakika utaweza kuuza huo mzigo wote bila pressure?” Juma akakaa kimya. Hakuwahi kufikiria hivyo. Khalid akaendelea:
Usichukue mkopo kwa sababu unaona opportunity… chukua mkopo kama una mfumo wa kurudisha.Sammy alizidi kumshawishi. “Bro, hii ni chance ya maisha… usikose.” Maneno hayo yalikuwa mazito. Baada ya siku mbili za mawazo… Juma alifanya uamuzi. Alichukua mkopo. Mwanzoni… Kila kitu kilionekana vizuri: Alipata mzigo mkubwa Wateja waliongezeka Mauzo yalipanda Juma alifurahi sana. “Nilikuwa naogopa bure,” alisema. Lakini ghafla… Mambo yakaanza kubadilika: Wateja wakapungua Baadhi ya nguo zikabaki bila kuuzwa Gharama zikaanza kuongezeka Na tarehe ya kulipa mkopo ikawa inakaribia…
NOTE: Mkopo bila plan ni mzigo. Hakikisha una uhakika wa soko kabla ya kukopa pesa ya biashara.
Juma alianza kupata pressure. Usingizi ukapungua. Simu ikaanza kupigwa mara kwa mara… “Pesa yetu lini?” Moyo wake ulianza kubana. Ndipo alipoanza kuelewa… Hii haikuwa tena biashara ya kawaida. Ilikuwa vita.Unapochukua mkopo, hauuzi tena kwa uhuru… unauza kwa presha.👉 Episode 8 itakuwa nzito sana 😳🔥 Juma atakutana na pressure kali ya madeni Ataanza kufanya maamuzi ya haraka (ya hatari) Na utaona jinsi biashara nyingi zinavyoanguka