Biashara Ni Vita

Sehemu 8

EPISODE 8: Presha ya Madeni

Biashara Ni Vita • Aisha Mtamu

Siku zilianza kwenda haraka kuliko kawaida. Kwa Juma… kila siku ilikuwa kama vita. Simu yake ilikuwa haikai kimya. “Bro, muda wa malipo unakaribia…” “Usisahau deni letu…” Kila call iliongeza presha. Biashara yake bado ilikuwa inaendelea… Lakini sasa haikuwa tena ile ya furaha. Ilikuwa ya kukimbiza deni. Presha ya deni inaweza kukufanya uuze… lakini pia inaweza kukufanya ukose mwelekeo. Juma alianza kubadilika: Alianza kushusha bei sana ili auze haraka Alianza kuchukua hata wateja wasio na uhakika Alianza kufanya maamuzi bila kufikiria sana Siku moja… Mteja alimtext: “Bro, nataka mzigo mkubwa, lakini sina pesa yote sasa… nitalipa baadae.” Zamani Juma angekataa. Lakini sasa… Alikuwa chini ya presha. Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa… Kisha akajibu: “Sawa, chukua… utanilipa.” Huo ulikuwa mwanzo wa kosa kubwa. Siku zikapita… Mteja hakulipa. Simu haipatikani. Juma alishika kichwa. “Kwa nini nimefanya hivi…” alijilaumu.

NOTE: Usifanye maamuzi ya biashara ukiwa chini ya presha. Mara nyingi maamuzi hayo huleta hasara zaidi.

Mambo yakazidi kuwa magumu: Deni halijapungua Faida imepungua Na hasara imeanza kuonekana Juma alikaa peke yake usiku mmoja… Akiangalia mzigo uliobaki. Moyo wake ulikuwa mzito. “Nilianza vizuri… imekuaje tena hivi?” alijiuliza. Ndipo alipokumbuka maneno ya Khalid… Biashara sio mbio… ni safari. Ukikimbia bila direction, utaanguka. Asubuhi iliyofuata… Juma alimtafuta Khalid. “Bro… mambo yameharibika,” alisema kwa sauti ya chini. Khalid alimwangalia kwa makini. “Kiasi gani umebakiwa nacho?” aliuliza. Juma akasema ukweli wote. Khalid hakumhukumu. Badala yake akasema: “Bado hujachelewa… lakini lazima ubadilishe strategy.” Khalid alimpa hatua 3: 1. Simamisha mikopo mipya kabisa 2. Uza mzigo uliopo hata kwa faida ndogo 3. Rudisha deni polepole bila panic Kwenye biashara, ku-survive ni muhimu kuliko kupata faida kubwa kwa haraka. Juma alisikiliza kwa makini. Kwa mara ya kwanza baada ya muda… Alipata utulivu kidogo. Lakini bado kulikuwa na swali moja kubwa: Je, ataweza kweli kutoka kwenye hili deni? 👉 Episode 9 inakuja na mabadiliko makubwa 🔥 Juma ataanza kujinasua kwenye madeni Atajifunza discipline ya hali ya juu Na biashara yake itaanza kurudi taratibu

Maoni

Hakuna maoni bado

Profaili

Alama ya uaminifu