SURA YA KWANZA.
JE UMEPATA KITU? • YUNUS SHABANI HANGA
SURA YA KWANZA.
Mwanamke…
Mwanamke…
Mwanamke…X3
Kabla hujawa mwanamke, utakuwa binti.
Na kabla hujawa mama, utakuwa mwanamke.
Chizi anachekesha, hasa pale akiwa sio ndugu yako.
Kama binti hajui, unadhani anaweza kujinasua kwenye mitego aliyowekewa?
Kijiji cha Manda kilikuwa kimetulia tuliii, vumbi liliruka kila upepo ulipopita, likikaa juu ya paa za nyasi na kwenye nyuso za watu waliokuwa wamezoea maisha yale kana kwamba hayakuwa na mbadala.
Sakina aliketi chini ya mti wa mkungugu, macho yake yakifuatilia kundi la wasichana waliokuwa wakipita njiani kuelekea kisimani. Vicheko vyao vilijaa hewani, lakini kwake vilisikika kama mbali sana kana kwamba vilikuwa vya dunia nyingine.
Alijishika goti, akiinamisha kichwa kidogo. Hakukuwa na mtu aliyemwambia wazi, lakini alijua, Maisha yake hayakuwa sawa na yao.
“Sakina!” sauti ya mama yake ilimuita kutoka ndani ya nyumba ya udongo iliyochoka. “Njoo hapa, kuna kazi bado.”
.......... INAENDELEA....